TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA.Na Vero Ignatus Arusha.

Mamalaka hiyo imekusanya shilingi bilioni 64.6, ikiwa imevuka malengo yake iliyojiwekea awali ya kuweza kukusanya shilingi bilioni 63.1.


Ongezeko hilo, ni sawa na asilimia 102, kulingana na meneja wa Mamlaka ya mapato  (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku.


Akizungumza katika mahojiano maalumu na blogu hii, bwana Mbaruku alielezea kuwa ongezeko hilo linatokana na majumuisho ya makusanyo ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.


“Ni kweli tumeweza kukusanya kiasi hichi cha fedha, nahii inatokana na kukua kwa mwamko wa ulipaji kodi mkoani hapa  japokuwa bado zipo changamoto kadhaa za baadhi ya wafanyabisahara kutokuelewa umuhimu wa kulipa kodi,” alisema meneja huyo.


Apili ametaja sekta ya utalii kuongoza katika ulipaji huo wa kodi.

“Tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kukwepa usumbufu usio na lazima,” alishauri meneja huyo.


Hata hivyo, Mbaruku aliweka wazi kuwa ofisi yake ilishindwa kufikia malengo ya ukusanyi wa mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16.

“Kwa mwaka uliopita malengo yetu yalikuwa kukusanya shilingi 329.5 lakini kwa bahati mbaya tulipata shilingi bilioni 324.6 tu”.


Akifanunua zaidi kuhusu makusanyo ya mwaka huu,  Mbaruku alisema kuwa kiasi cha bilioni 30.3  zilitokana na makusanyo ya ndani wakati shilingi bilioni sita zilitokana na malipo ya ushuru.


Aidha, Mbaruku ameongeza kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na maofisa wa jiji la Arusha kuanza kukusanya makusanyo ya kodi za majengo.


Kulingana na meneja  huyo wa TRA, ofisi yake inalenga kukusanya kodi kutoka kwenye majengo 20, 536 mkoani hapa. Mamlaka ya mapato mkoni Arusha(TRA) imevuka lengo la makusanyo yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.“Nia yetu ni kuanza kukusanya kodi kutoka kwenye majengo hayo, na tayari tumeshafanya mawasiliano na maofisa wa jiji na kuweza kubainisha majengo hayo,” aliongeza meneja huyo wa TRA mkoani Arusha.


Powered by Blogger.