Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea kwa michezo mbalimbali kupigwa leo Jumapili ya Septemba, 2 na mmoja wa michezo huo ukiwa ni mchezo wa Tottenham Hotspur iliyokuwa mwenyeji wa Manchester City katika dimba la White Hart Lane.
Mchezo huo umemalizika kwa Tottenham kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila, magoli ya Tottenham yakifungwa na Aleksandar Kolarov kwa kujifunga dakika ya tisa na Dele Alli dakika ya 37 ya mchezo huo.
Ushindi wa Tottenham umemaliza utemi wa Manchester City kwani katika michezo sita iliyokuwa imecheza kabla ya leo ilikuwa imeshinda michezo yote, na huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Manchester City kufungwa tangu awasili kocha Pep Guardiola.