Tizama matokeo na msimamo wa ligi Kuu Primus League Burundi wiki ya 5

Ligi Kuu ya Primus League Burundi imeingia kwenye wiki yake ya 5 huku kuna mabadiliko makubwa  katika msimamo wa ligi tofauti na wiki ya 4. Mjini Bujumbura Buja City inaendelea kupoteza kwa kuridhika kupigwa vikali bao tatu kwa moja dhidi ya Magara Star (1-3), LLB inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa kupata ushindi wa bao moja bila dhidi ya Inter Star (1-0), timu kama Olympic Star na Flambeau zimeshindwa kujitetea mbele ya mashabiki zao kwa kupoteza pointi huku Les Lierres imecharazwa vikali kwa bao nne bila dhidi ya Musongati.

Matokeo ya wiki ya 5: 

Jumamossi, 08/10/2016:
-Buja City 1-3 Magara Star.
-LLB 1-0 Inter Stars
-Ngozi City 2-0 Rusizi FC
-Olympic Star 0-1 Muzinga
Flambeau de l'Est 1-2 Messager Ngozi.
-Musongati 4-0 Les Lierres.

Jumapili  09/10/2016:

-Messager Bujumbura 0-2 Athletico Olympic.
-Aigle Noir 0-0 Vital'o

Msimamo wa Ligi Kuu Primus League wiki ya 5:

1.LLB: Pointi 15 na bao 6
2.Athletico Olympic: pointi 13 na bao 14 
3.Inter Stars: pointi 12 na bao 3
4.Musongati FC: pointi 9 na bao 5
5.Messager Ngozi: pointi 9 na bao 1
6.Aigle Noir: pointi 8 na bao 2
7.Ngozi City: pointi 6 na bao 1 
8.Flambeau de l'Est: pointi 6 haina bao
9.Muzinga: pointi 6 na bao -4
10.Les Lierres: pointi 5 na bao -2
11.Rusizi FC: pointi 5 na bao -4
12.Vital'o: pointi 4 na bao -1
13.Magara Star: pointi 4 na bao -3
14.Olympic Star: pointi 4 na bao -7
15.Messager Bujumbura: pointi 2 bao -6
16.Bujumbura City: pointi 1 na bao -
Powered by Blogger.