Tizama picha ya mechi ya kusisimua kati ya LLB dhidi ya Inter Star 1-0


Ligi ya Primus League imeingia kwenye wiki yake ya 5 wiki hii na mechi zimepangwa kwenye nyakati tofauti huku mechi ya kusisimua imekuwa ni kati ya LLB dhidi ya Inter Star ambapo timu zote zimekuwa kileleni na pointi zote 12.
Kama tunavyo fahamu katika soka timu mbili zikikumbana matokeo lazima ni sare ao mshindi umoja, basi timu ya LLb imeonekana kumiliki mpira zaidi kipindi cha kwanza wamepata nafasi kubwa ya kufunga ila hawakuitendea ipasavyo. Kipindi cha pili ndipo LLB imerudi tena kuwa juu na kufanikiwa kupata goli moja la ushindi kupitia mshambuliaji wao hatari ajulikanae kwajina la LambaLamba.
Katika Mchezo huo mchezaji Rashidi Leon ambaye ndie naodha wa LLB amepatwa na jeraha usoni ila haikumziwia kuendelea na kusaidia timu yake kupata ushindi wa bao moja bila ya Inter Star na kuongoza Ligi kwa mda wiki hii.Powered by Blogger.