TAMASHA LA GOSPEL FESTIVAL LAFANA ARUSHA

Wa pili kushoto ni Mkrugenzi wa habari maalum Radio Bw. Leonard George, kwanza kushoto Mch Marandu Kulia ya Mkurugenzi ni Mch Rukiya Mwenyekiti wa Bodi Habari Maalum kulia kwake ni Mgeni Rasmi Ask: J. Laizer wa Naivera Apostolic Church, na wa kwanza kulia Mch. Orche Mgonja wa Lhu Pentekoste  wakiwa anafuatilia kwa karibu kinachoendelea katika tamasha la Gospel Festival lililofanyika katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid (stadium) Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na Vero Ignatus Arusha.

Tamasha lililoandaliwa na Taasisi ya Kidini Radio Habari maalum(R.H.M) Mkoani Arusha lijulikanalo kama (Gospel Festival) limefanyika jumapili katika Uwanja wa Shekh Amri Abeid (Stadium)na kuhudhuriwa na waimbaji mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi ya Tanzania.


Akizungumza mkurugenzi wa wa Taasisi hiyo ya kidini( R.H.M) Leornad George amesema kuwa lengo kuu la kufanya tamasha hilo ni kuleta umoja wa makanisa na, kwakupitia tamasha hilo itaondoa ule ugumu wa na fikra potofu kuwa kanisa fulani ni bora kuliko jingine.


"Unajua Mungu anatuhitaji sisi wote tumsifu yeye maana yeye ndiye Muumbaji wetu,hakuna sababu ya wewe kupewa punzi ya uhai na Mungu kisha ukae kimya bila hata kuinua sauti yako na kumsifu yeye,maana hata baada ya maisha ya hapa duniani kupita bado tukifika kwawe kusifu kutaendelea milele na milele"alisema Leonard.


Kwa upande wake meneja wa kituo cha fm 97.7 ndugu Daniel Reuben Magulu amesema kuwa wamewakaribisha waimbaji kutoka makanisa mbalimbali Arusha na muitikio ulikuwa mkubwa,na amesema kupitia tamasha hilo zile tofauti za waimbaji kujinitenga hazitakuwepo tena na wote tutakuwa ndugu wamoja maana tunamtumikia Mungu.


"ifikie mahali kila mmoja atambue kazi ya mwenzie bila kuwa na ubaguzi huku kila mmoja akimuhesabu mwenzie ni bora kuliko yeye"alisisitiza Magulu.


Aidha ameainisha  waimbaji waliohudhuria ni kutoka nchi mbalimbali duniani,Sweeden,Finland,Dermack,Ufaransa,Italia ,Canada na wenyeji Tanzania ambapo amesema nchi nyingine za Afrika ya Mashariki Kenya ,Uganda,Rwanda,na Burundi watahudhuria tamasha lijalo kwa sasa wameona waanze na hawa.


Magulu amefafanua kuhusu( Gospel Festival ) kuwa ni sherehe ya mavuno ya Injili,ametoa wito kwa makanisa yote na kusema kuwa Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu "Tuwe na umoja ili adui asipate nafasi"alisisitiza".

Powered by Blogger.