responsive ads

Studio 4.12 ya Dully Sykes kuwasimamia wasanii hawa wawili raia wa Uholanzi

Hit maker wa ‘Inde’ na mtayarishaji wa muziki, Prince Dully Sykes Ijumaa hii amewatambulisha wasanii wawili ‘Martha na Amy’ raia wa Uholanzi ambao watakuwa chini ya studio yake ya 4.12.
2016-10-20-13-03-58-993-1
Dully Sykes na wasanii wake
Akizungumza na mishe mishe media Ijumaa hii akiwa katika studio hiyo iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es salaam, Dully alisema vipaji vya wasanii hao vimeifanya studio yake kuchukua jukumu la kuwasimamia ili kuhakikisha wanafika sehemu fulani katika muziki wa Tanzania.
“Hawa ni wa wasanii wa studio yangu 4.12, mmoja anaitwa Martha na mwingine Amy, nimekaa nao nikaona kwenye muziki wao kuna ladha fulani ambayo ni nzuri, kwa hiyo kama studio ya 4.12 nikaona nisiishie kufanya nao kazi tu, pia niwasaidie kuhakikisha wanafika sehumu fulani,” alisema Dully Sykes.

Amy
Aliongea,”Mpaka sasa tayari wana ngoma mbili, moja wamefanya na Barakah The Prince na nyingine wamefanya na mimi, lakini wiki ijayo itaanza kutoka kazi ambayo wamefanya na Barakah The Prince. Pia video tunapanga kwenda kushoot Uholanzi ili kupata kitu kizuri zaidi,”

Martha
Dully Sykes alisema wasanii hao wamependa kufanya muziki wa Tanzania na wamekubali kuimba kwa lugha ya Kiswahili.
middle 300x250
Powered by Blogger.