Shamba la bangi hekari 8 labainika Arusha, viongozi wa eneo hilo wahusishwa

 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Pastory Mnyeti ameamuru kukamatwa kwa kwa diwani wa kata ya Lemanyata Losyeku Kilusu Arusha, wenyeviti wa vitongoji saba, wenyeviti wa vijiji watatu kwa kujihusisha na kilimo cha bangi pamoja kuuza. Mnyeti amemtaka diwani ajisalimishe polisi kutokana na kata yake kukutwa na Hekari zaidi ya nane za bangi. DC Mnyeti amesema…….
wenyeviti wa kitongoji, watendaji wa vijiji hii ni biashara yao namba moja haiwezekani mashamba ya bangi yanalimwa, watu wanalima mnaona, mpaka yanafikia kimo hiki mnaona, mpaka mimi mkuu wa wilaya nakuja mpaka huku nyinyi pengine hamna taarifa za hiki kilimo’
OCD nakuagiza kamata watu hawa wote, weka ndani mpaka wakuambie nani analima hii bangi, maana kwanza hawako tayari hata kusema, halafu hili zao sitaki kuliona msikate kwa chini mng’oe kabisa’:- DC Mnyeti
Powered by Blogger.