SERIKALI:IPO TAYARI KUSAIDIA MACHINJIO ARUSHA


Na Vero Ignatus Arusha
Serikali imesema iko tayari  kusaidia machinjo ya mifugo ya Arusha meat ,kuanzisha kiwanda cha kuchakata ngozi ili kusaidia kuinua pato la taifa 

Akizungumza hayo  alipoenda kutembelea Machinjio hayo kuangalia shughuli mbalimblai zinazofanywa na machinjio hayo ,Naibu waziri wa Mifugo ,Uvuvi na Ufugaji Wiliam Ole Nasha,alisema serikali ipo tayari kusaidia machinjio hiyo kuanzisha kiwanda hicho ilikuwezesha kukuza soko la ajira nchini 


Pia  imesema itazungumza na  mifuko ya hifadhi ya jamii nchini ili iweze kuwekeza katika kiwanda hicho ambacho kitatoa ajira nyingi kwa vijana.


“Serikali ya awamu ya tano inatoa msukumo mkubwa wa kuwekeza  kwenye  viwanda  haswa vinatumia malighafi "alisema Ole Nasha

"Naomba kuanzia sasa muangalie namna ya kujenga kiwanda cha kuchakata ngozi inayotokana na mifugo mnayoyanjiacha hapa kwa kuwa mna eneo kubwa la kutosha ambalo halitumiki”

Naibu waziri huyo ,pia alitoa ushauri kwa uongozi wa machinjo hayo kuangalia namna ya kutengeneza vyakula vya kuku kupitia kuchakata mifupa na damu za mifugo 


Pia amesema, ilisoko la walaji liongezeke ipo wajibu kwa machinjio hayo kuangalia namna ya kuongeza thamani ya nyama kwa walaji wake 

Kwa mujibu wa Ole Nasha Tanzania ni nchi ya pili katika  bara la Afrika kwa wingi wa mifugo lakini haina viwanda vya kuchakata ngozi na kwamba ngozi inayotumika  katika gereza la Karanga liliko mkoa wa Kilimanjaro inatoka nchini Kenya.

Hata hivyo ,amesema kanda ya kaskazini imekuwa ikipoteza mapato yake yatokanayo na uuzwaji wa mifugo hiyo huku mifugo mingi ikiuzwa nchini kenya 

Upande wa kaimu meneja wa Arusha Meat,Joseph Singuya amesema machinjio hiyo ina uwezo wa kuchinja ng’ombe kati ya 400 mpka 500 kwa siku lakini kutokana na wilaya ya Arumeru iliyopo jirani na eneo hilo wanachinja ng’ombe 140 na mbuzi 130
Powered by Blogger.