Rapa wa muziki wa Bongo Fleva, Country Boy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kubwagiwa mtoto na mzazi mwenzake.

eNewz ilimtafuta Counrty Boy na kuzungumza nae kuhusu sakata hilo na alisema kuwa amejifunza kuwa kuna umuhimu kwa mapenzi ya baba kwa mtoto, imezoeleka kwa wazazi wa kiume hutoa pesa tu ya malezi pasipo kuhangaika kwa malezi lakini kwake ameona kuna umuhimu wa mapenzi ya baba kwa mtoto.
“Nimejifunza mapenzi ya mama pia nimegundua umuhimu wa mama uko wapi, nimegundua love ya mtoto na umuhimu wa baba. Nimegundua kuwa majukumu yangu natakiwa kutumika serious sana, Naji'feel' kama blessing man”
Pia Country Boy alizungumza kuwa haoni tatizo kubwa sana kwake pale mtoto wake anapokosa malezi ya pande zote mbili (Malezi ya Mama) na kuamini kuwa siku moja mtoto wake atakuja kuwa mtu mkubwa sana.
Powered by Blogger.