Rais wa Ufilipino ajifananisha na Hitler, aahidi kuwaua watumiaji wa dawa za kulevya mil 3

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amejifananisha na kiongozi wa Nazi, Adolf Hitler Ijumaa hii kwa kusema kuwa atafurahi kuwaua watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya milioni 3 nchini humo.
rodrigo-duterte-speech-defense-sporting-arms-show-megamall-mandaluyong-20151111-002
Kauli hiyo imesababisha hasira kwa makundi ya wayahudi nchini Marekani ambayo inaweza kuisababisha Marekani ichukue maamuzi mazito dhidi ya kiongozi huyo wa Ufilipino. Duterte aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakosoaji wamekuwa wakimchukulia kama binamu wa Hitler.
Akieleza kuwa Hitler aliua mamilioni ya wayahudi, Duterte alisema, “Kuna mateja milioni 3 (Ufilipino). Nitafurahi kuwachinja. Kama Ujerumani ilikuwa na Hitler, Ufilipino itakuwa na mimi.”
Mshauri wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya halaiki, Adama Dieng, alieleza mashaka yake juu ya kiongozi huyo na kumtaka arekebishe kauli zake. Mwezi August, Duterte alitishia kuiondoa Ufilipino kutoka Umoja wa Mataifa baada ya kumtaka aachane na mauaji dhidi ya watumiaji wa dawa za kulevya.
Tangu Duterte aingie madarakani June 30, zaidi ya watu 3,100 wameuliwa, wengi wao wakiwa watumiaji na wauzaji wa unga.
Powered by Blogger.