Rais Magufuli aagiza kutumbuliwa maofisa wawili uwanja wa ndege

Rais Dkt John Pombe Mgufuli ameagiza kushughulikiwa maofisa wawili wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, waliompa taarifa za uongo mwezi Mei mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza uwanjani hapo.
14590972_198503040584117_3486503061885550592_n
Rais Magufuli amechukua uamuzi huo Jumatano hii wakati alipomsindikiza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alikuwa akiondoka nchini baada ya ziara ya siku tatu.
Aliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza uwanjani hapo kwa mara nyingine na kujionea mashine zilizokuwa hazifanyi zikifanya kazi.
“Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona, lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua,” amesema Magufuli.
Maofisa walio matatani ni pamoja na Lilian Minja na Novia Maduka.
Powered by Blogger.