Primus League matokeo, Atletico inaitambia LLB, Messager Ngozi imeshindwa kujitetea na Inter Star inazidi kudidimia

Primus League imeendelea wiki hii kwa kishindo huku timu mbali mbali zikishindwa kujitetea na zingine zinazidi kufanya vizuri.
Baada ya kufunguliwa kipigo dhidi ya Messager Bujumbura wiki tatu iliyo pita, pointi moja mechi tatu, ndizo takwimu ya Inter Star baada ya miamba hiyo kuonesha kuwa imerudisha heshima yake kwenye ligu kuu mechi za mwanzo, kwasasa Inter Star inazidi kudidimia mpaka kufikia kucharazwa vibaya na Musongati ya mkoani Gitega kwa bao tano (5-0) bila jibu. Inaonekana Inter Star haijawa sawa na kikosi cha kwanza na pia kwenye safu ya ushambuliaji.

Atletico Olympic licha ya kuongoza ligi kuu kwa mda wiki iliyo pita, inazidi kuwa kileleni wiki hii na kuakikisha imewaacha mbali wapinzani kwa kuwacharaza katika mechi ya leo bao moja bila ya LLB (1-0).

Messager Ngozi imeonekana kuwa vizuri wiki mbili zilizo pita ila wiki hii imepigwa namshangao kwa kutoka suluhu na Rusizi.
 Klabu ya mkoani Ruyigi, Flambeau de l'Est licha ya kuonekana wa babe dhidi ya Vitalo wiki iliyo pita na kufanikisha kupata pointi moja dhidi ya wabingwa watetezi Vitalo, leo imeambulia sufuri kwa kucharazwa na Musongati ambayo ni timu kwasasa inazidi kuwa bora zaidi.

Haya ndio Matokeo ya Primus League wiki hii :

-Messager Ngozi 0_0 Rusizi f.c
-Flambeau de l'est 0_1 Musongati
-Aigle noir 3_0 Ngozi city
-Inter star 1_1 Muzinga f.c
-Magara star 0_3 Messager Bujumbura .
-Olympic star 2-2 Buja City.
-Atletico Olympic 1-0 LLB.Academic

- Vitalo 2-0 Les Lierres 


Powered by Blogger.