responsive ads

Mwimbaji Koffi Olomide Achukua Dakika Moja Kuwaomba Msamaha Wakenya Kwa Kumpiga Mwanamke

Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye mwezi July aliwasili  Nairobi
Kenya  akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show
na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake
wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo
hicho.Koffi Olomide aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili
kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali,  na hiyo ilielezwa kuwa kuachiwa
kwa koffi Olomide kulikuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa
hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na
tukio alilofanya JKIA.Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi
Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia
kipindi cha Television cha Churchill Show amewaomba msamaha wakenya na
mashabiki wake kwa ujumla na kusema …….’Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa
upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na
maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu
licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide
middle 300x250
Powered by Blogger.