MWANDISHI WA BBC ATUA AZAM FC KUWA MENEJA MKUU


Leo October 6, klabu ya Azam FC imemtambulisha Adbul Mohammed kuwa General Manager wa klabu hiyo ambapo mbali na utambulisho huo wameeleza lengo kuu la kumpa wadhifa huo ndani ya timu yao.
C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba amesema lengo la kumwajiri Abdul kama General Manager ni kuhakikisha mabingwa hao wa kombe la Kagame wanapiga hatua mbele kwenye upande wa professionalism.
img_0267
“Tunamtambulisha mwenu Abdul Mohammed, rasmi ni mwanafamilia wa Azam FC, anaingia moja kwa moja kwenye secretariat ya Azam FC lengo ni kuhakikisha klabu yetu inapiga hatua kwenda kwenye professionalism,” amesema Kawemba wakati akimtambulisha Abdul Mohamed.
“Atakuwa ni General Manager wa klabu yetu akishughullika na masuala ya kila siku yanayohusu klabu yetu. Tunamkaribisha kwetu kwa nia moja tukiamini uzoefu wake na weledi wake utatusaidia Azam FC kuondoka katika hatua tuliyopo kwenda hatua nyingine ya mbele zaidi.”
Abdul amesema atahakikisha muundo na muonekano wa Azam unabadilika na kuwa wa kiueledi.
“Nimekuja kwenye klabu ya Azam kwa ajili ya kufanyanao kazi kujaribu kuona tunaivusha au kubadilisha muonekano na muundo wa klabu kwenda kwenye hali ya weledi zaidi,” amesema mwandishi huyo wa zamani wa idhaa ya Kiswahili ya BBC.
“Azam ni klabu changa lakini ni miongoni mwa klabu kubwa Tanzania, tunataka kuwapa mashabiki wetu aina flani ya utofauti ambao hauwezi kupatikana kwenye vilabu vingine isipokuwa Azam.”
Powered by Blogger.