Mwambusi Ataiongoza Yanga Kwa Muda, Lwandamina Ataanza Kazi Mwezi Ujao

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi atakiongoza kikosi cha Yanga katika mechi zilizobaki hadi hapo kocha mkuu mpya atakapoanza kazi.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema George Lwandamina raia wa Zambia ataanza kazi rasmi Novemba Mosi.

Tayari Lwandamina yuko jijini Dar es Salaam na Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yanga.
“Mwambusi ndiye ataendelea na kikosi, mambo mengine yakikamilika Lwandamina ataanza kazi,” alisema.

Awali ilielezwa kwamba Pluijm atakuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga kabla ya mwenyewe kuamua kujiuzulu.
Powered by Blogger.