Hatungimana Aline wengi wanamfahamu kwajina la Media, ni muigizaji wa filamu wa Burundi Movie katika kundi la Tambwe The Great Films awali ameigiza katika filamu itwayo ZAWADI YA MWAKA akiwa kwenye kundi la The King Great Films ya mjini Bujumbura.

Mwanadada mrembo Media amedai kuwa ye ndiye muigizaji bora wa kike na amewataka wengine wawe makini kwasababu amejipanga vizuri mwaka huu na filamu nyingine itakuja kumtambulisha kimataifa zaidi.
Kampuni Tambwe The Great Films hipo kwenye maandalizi ya filamu mpya ambayo imewashirikisha ma staa kibao kama Jay Fire, Divine na Chany Queen huku katika kundi ilo kuna warembo wengi kama Media na wengine watakao itendea haki filamu hiyo.

Media amesema kuwa filamu yao mpya itakuwa ni filamu kubwa katika tasnia ya filamu. Nyota huyo katika tasnia ya filamu Tambwe The Great Films Hatungimana Aline ‘Media’ ipo tayari kuingia sokoni na kutengeneza kazi  katika viwango vya kimataifa, kazi hiyo mpya inakwenda kusaka tuzo kubwa kabisa duniani.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top