Mtandao wa mtoboa macho wanaswa

Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, imefanya operesheni katika maeneo ya katikati na pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam na kuwakamata watuhumiwa 87 wa makosa mbalimbali, wakiwemo waliokuwa kwenye mtandao wa uhalifu wa mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salim Njwete (34) maarufu kama ‘Scorpion’.
20160404031823
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu hii, Kamanda Sirro amesema watuhumiwa wengine wanadaiwa kuvunja nyumba na kuiba na wengine walipatikana na gongo lita 148, bangi kete 95 na puli 48.
“Watuhumiwa hao walipatikana na makosa mbalimbali yakiwemo kuvunja nyumba usiku na kuiba ndani kuvuta, na kuuza bangi, kuuza na kunywa gongo, kupiga debe, uzembe na uzururaji,” alisema Kamanda Sirro.
Njwete (Scorpion) alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwishoni mwa wiki, kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Ally Mrisho.
Aidha kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao, wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Mbagala, Buguruni, Kiluvya, Gongo la Mboto, Tandika, Ukonga, Banana, Kunduchi, Keko, Kawe.
Powered by Blogger.