TANGAZO
Msanii wa WCB, Raymond, amedai kuwa wakati mwingine anapofuata sana misingi ya kazi, baadhi ya watu hudhani kuwa anaringa, kitu ambacho anadai hawezi kuwa nacho.
14360167_1213814638693077_116105249617346560_n
“Kwa mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha, aniombe namba ya simu,” Ray aliiambia mishe mishe media.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.
“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi sababu ndio unaonipa hela,” aliongeza.
Muimbaji huyo ametajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha Best Breakthrough Act.
Msikilize zaidi hapo chini.

kumbuka biashara ni matangazo kama wewe ni msanii au mfanya biashara na ungependa kazi yako ionekane kenye website hii wasiliana nasi kwa no; +255714903603

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq
 
Top