Msanii wa Tanzania “DJ DAVIZO” Kumshitaki Msanii wa Kenya “DUFLA” kwa Wizi

Wizi ni wizi tu na unatafsirika kama Wizi ambao ni Makosa katika Jamii Kuiba, Ukiiba kijanja Usipokamatwa Umetoboa ila ukikamatwa Inaegemea Upande wako.
Well inaweza isiwe kubwa sana kwenye Muziki wa Afrika Mashariki ila ingekuwa Marekani Msanii wa KenyaDufla Diligon, angetakiwa kumlipa kiasi kikubwa sana cha Pesa Msanii wa Arusha Tanzania, Dj Davizo kwa Ku-copy n Paste Video yake ya Napenda Dancehall.
DJ Davizo
DJ Davizo
Mnamo September 1-2016, Davizo aliachia Video ya wimbo wake Uitwao Napenda Dancehall ambao Video yake iliongozwa na Kampuni ya Wanene Entertainment, Lakini cha Kustaajabisha ni kwamba MnamoOctober 12-2016 Msanii wa Kenya Dufla Diligoni kutoka Grandpa Records, Ameachia Video ya wimbo wake uitwao Biringisha ambapo Ameiba Idea ya Video ya Davizo kwenye Kila kitu.

Dufla Diligon
Ukiiangalia Video ya Dufla, utagundua kwamba yeye na Director Wake ambaye ni Young Wallace, Wameibia kila Kitu kuanzia Mavazi ya Msanii na Dancer, Baadhi ya Style za Dancers kwenye Kucheza, Editing Style ya Video, Video Background, Uchaguzi wa Watu wa Kutokea Kwenye Video (Models), Wameweka mpaka Mmasai kama Davizo alivyoweka na Mambo Kibao.
Sasa Dj Davizo amebisha Hodi kwenye Studio za VMGAFRICA TV na Kulalamikia Kitendo cha Msanii huyo wa Kenya Kuonyesha Kuishiwa na Ubudifu na hatima yake Kuishia Kuiga kila kitu kwenye Video yake.
Hata hivyo Davizo amesema Ana Mpango wa Kumfungulia Msanii huyo wa Kenya Mashtaka kwa wizi wa wazi wazi.
MTAZAME DJ DAVIZO KWENYE EXCLUSIVE INTERVIEW NA DJHAZUU
Powered by Blogger.