Msanii wa muziki, Addul Kiba baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Bayoyo’ anajipanga kuachia wimbo mpya akiwa amemshirikisha mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’, Mr Blue.

abdul-kiba
Akiongea na mishe mishe media wiki hii, Abdul Kiba amesema tayari ameshafanya maandalizi ya kazi hiyo mpya na sasa anachosubiria ni kuangia location kwa ajili ya kuanza kushoot video ya wimbo huo.
“Baada ya wimbo ‘Bayoyo’ kufanya vizuri najipanga kuingia location kwa ajili ya kushoot video ya wimbo wangu mpya nikiwa nimemshirikisha Mr Blue. Wimbo ni mkali sana lakini kwa sasa nisingependa kuweka wazi jina la wimbo ila mnachotakiwa kujua soon tunaingia location kushoot video,” alisema Abdul Kiba.
Muimbaji huyo amesema kwa sasa hata kaa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya kutokana na game la muziki kuwa na ushindani mkubwa kwa sasa.
Powered by Blogger.