Ray-C-and-Lord-Eyez
Rapa huyo mwenye makazi yake mkoani Arusha, amesema anamuombea mwanadada huyo kwani kwa matatizo aliyonayo ni kama maradhi hivyo hayaponi kwa siku moja.
“Sijakutana naye wala hatuongei ila namuombea Mungu kwani tatizo lile ni kama maradhi mengine hivyo haliwezi kuisha kwa mara moja linachukua muda, anahitaji maombezi na mimi namuombea kama navyojiombea mimi nifanye kazi zikamilike tukutane kwenye show huko” Lord Eyez alikiambia kipindi cha Enewz cha Eatv.
Pia Lord Eyez amesema bado anaona Ray C ana nafasi ya kufanya vizuri kwenye muziki kwa kuwa hakuna msanii kwenye muziki anayefanya muziki wa aina yake.
“Leo hii kwenye muziki hatumuoni mtu kama Ray C, mpaka sasa hakuna mtu kama Ray C hivyo chumba chake kwenye muziki bado kipo kinamsubiri arudi tu,” alisema Lord Eyez.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top