Msanii wa Bongo Flava aliyetamba na wimbo ‘Sina Raha’ Sam wa Ukweli amefunguka sababu iliyomfanya akae kimya kwa kipindi kirefu.

sm-pic
Muimbaji huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa lebo yake ya Al Jazeera ndiyo iliyosababisha awe kimya kwa muda mrefu.
“Nilitaka kuvunja mkataba na lebo ya Al Jazeera kutokana na kuona hakuna kazi iliyokuwa inafanyika, hivyo nilitaka kuwa huru lakini ilishindikana na niliambiwa nilipe shilingi milioni 100 kama nataka kutoka kwenye lebo hiyo, hali hiyo ilinifanya nikae kimya kwa muda mrefu;” amesema Sam.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa mkataba wake na lebo hiyo umeshamalizika na sasa yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote.
Powered by Blogger.