MSANII RAYMOND AWEKA WAZI TARATIBU ZAKUFUATA ILI AKUANDIKIE WIMBO

Mkali wa wimbo ‘Natafuta Kiki’ Raymond aka Rayvanny amesema kwa sasa hana tena ushikaji kwenye kumwandikia mtu wimbo.

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya WCB, amesema ili akuandikie wimbo unatakiwa kuzugumza na uongozi wake huku akikutaadharisha kujipanga vizuri katiika malipo.

“Zamani nilikuwa nikienda kuandika nyimbo utasikia shika hii hela sasa hivi, ukisema nikiandikie nyimbo sasa hivi sijui itakuwaje,” Rayvanny akiambia kipindi cha Uhurufleva kinachoruka Uhuru FM. “Labda niseme ngoja tusaidiane naye kuandika lakini siyo mtu aniambie nimwandike halafu atanilipa hela, kwa sababu nishaijua biashara ya muziki, nimeshaona utamu wa hela ya shows, so ni hela nyingi zinakuja kutokana na muziki kwa hiyo ukiniambia nikuandikie wimbo najua ni faida gani ambayo nitakupa, kwa hiyo lazima niangalie mara mbilimbili,”

Aliongeza, “Pia management haijaniruhusu kudeal na kazi yoyote ambayo ipo nje ya WCB, kwa sababu tayari nimeshakuwa chini yao. Mtu akitaka ngoma niandike, anapiga simu tu kwa uongozi halafu mimi nikiambiwa nikuandikie nakuandikia.

Muimbaji huyo anasifika kwa kuwa na vipaji vingi kikiwemo cha kuandika nyimbo.
Powered by Blogger.