Msanii mkongwe aliyechomoza toka THT, Amin, amepata mtoto ambaye amempa jina lililozua maswali mengi.


Mtoto huyo mwenye umri wa miezi minne amempa jina la "Wairith" jina ambalo amedai kuwa maana yake ni sarafu ya mji wa Makka.
Amin akitoa sababu za kumpa mtoto wake jina hilo alisema "Mazingira aliyopatikana mwanangu yalikuwa magumu sana, mwanangu alimsumbua sana mama yake, achana na ile mimba ya kwanza ambayo ilifia tumboni. Hivyo nimempa mwanangu jina la sarafu ya Makka kwa sababu sarafu hiyo kuishika pale ilipo inabidi ufanye kazi kubwa sana".
Jina hilo la Wairith ni tofauti na jina halisi la sarafu ya Makka, kwani Makka wanatumia sarafu ya Saudi Arabia iitwayo Riyal lakini mwenyewe amelisifu jina hilo kiasi cha kusema kuwa mara nyingine wakienda hospitali hupewa ofa ya kutibiwa bure kwa sababu ya jina hilo.
Powered by Blogger.