Msanii Juma Nature asema Singeli ni muziki wa kihuni, hautodumu

Singeli ni muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa.
13549629_1051489578275396_561623312_n
Licha ya kuonekana kufanya vizuri mpaka kufikia kiasi cha kuwashawishi wasanii wa muziki mwingine kujiingiza katika muziki huo, wapo baadhi ya watu wameonekana kutokuwa na imani nao.
Nilifanikiwa kupiga story na msanii mkongwe wa Bongo Flava, Juma Nature, mapema wiki hii katika studio zake za Halisi Records kuhusu muziki huo ambapo yeye alidai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.
“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema. “Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumb*vu pumb*vu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature ambaye hivi karibuni aliachia ngoma yake mpya iitwayo Mtumba.
Powered by Blogger.