Dayna Nyange amefunguka kuwa atakuwa tayari kuwa chini ya lebo yoyote endapo watakubaliana na masharti yake.
dayna-nyange
Hitmaker huyo wa ‘Komela’ amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kikubwa nachoangalia ni sababu, kabla sijajiunga na lebo yoyote lazima niwe na vitu vyangu ambavyo navitaka na wao wanavitu vyao wanavyotaka.”
“Record label ni studio tu ambao watu watakuwa wanasimamia kazi zangu ni kitu ambacho mimi mwenyewe ninaweza nikaenda sehemu yoyote nikafanya kazi zangu. Kuna vitu vingi sana kabla hujaingia kwenye lebo yoyote kama kuna makubaliano mazuri yatakuwepo basi tutafanya kazi,” ameongeza.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amekanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Idris Sultan zaidi ya kuwa marafiki tu.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top