Msanii Alikiba akanusha kutumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania 2016

Alikiba amekanusha taarifa zilizoenea kuwa atatumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika Jumamosi hii mjini Mwanza.
miss-tanzania
Taarifa hizo zilizosambaa zimedai kuwa Alikiba na Christian Bella ndio wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo lakini Kupitia mtandao wa Instagram, hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Aje’ ameandika, “Taarifa Muhimu : Napenda Kuwajulisha Ya Kuwa Sitakuwepo.”
Tamasha hilo litakuwa likifanyika mkoani humo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo nchini.
Powered by Blogger.