Msani Davidson anatarajia kusaini mkataba na SAIDI NTIBAZONKIZA

Msanii Gashano David akijulikana kwajina la Davidson kutoka Burundi mwenye makazi yake Afrika Kusini, anatarajia kusaini mkataba na mchezaji wa soka wa kimataifa naodha wa zamani wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Saidi Ntibazonkiza ambaye kwasasa anaishi Ufaransa.

Mkali wa Nukobimeze inayo zidi kufanya vizuri Afrrika Kusini na afrika mashariki, Davidson kwasasa yupo Swaziland na siku chache anatarajia kutua  Durban New Germany ki kazi ya muziki.

Davidson kwasasa anazidi kukubalika sana kwenye game ya muziki na ni msani ambaye apendeleyi kuongelea mambo yake sana huku kazi zake akiziendesha  kimya kimya. Msanii huyo ameiakikishia Africanmishe kuwa mwanzoni mwa mwezi Decembea atajielekeza Ufaransa kwa kukamilisha na kusaini mkataba na manager mpya ambaye ni maarufu sana Burundi akijulikana kwajina la Saidi Ntibazonkiza, ambaye ni naodha wa zamani wa timu ya taifa ya Burundi pia mchezaji wa zamani wa Caen ya Ligue 1 Ufaransa, msimu uliyo pita. 


Powered by Blogger.