MKONGWE wa Bongomovies RICH RICHIE ATAKA WASANII WAACHWE HURU ILI KUPATA UHALISIA

MKONGWE wa Bongomovies, Single Mtambalike "Rich Richie" amesema umefika wakati sasa wasanii kuwa huru katika kazi zao ili waweze kuigiza kwa uhalisia wa matukio husika. Alisema kuwa wasanii wamekuwa wakishindwa kuonyesha vipaji vyao kutokana na wasimamizi wa kazi za sanaa kufungia baadhi ya kazi zao kwa madai kwamba hazina maadili. Richie alisema kuwa hatua hiyo inawashusha na kupoteza uhalisia wa matukio wanapokuwa wakiigiza hivyo kuna haja ya kuangalia upya ili wawe huru kufanya kazi kwa kujinafasi. “Wasanii tuwe huru ili tupate uharisia kwani sio kila Movies inaangaliwa na familia, wanachotakiwa wao ni kuweka tu viwango kwamba filamu fulani ni ya miaka 18… hii ni kazi lakini pia ni biashara,” alisema Richie.
Powered by Blogger.