Mikufu, pete alizoibiwa Kim Kardashian ina thamani mara 6 ya bajeti iliyotengwa na serikali kusaidia mfuko wa sanaa Bongo

Ukitaka kujua kuwa alichopoteza Kim Kardashian jijini Paris, Ufaransa baada ya kuvamiwa kwa mtutu wa bunduki na watu watano, kigeuze kwa shilingi ya Tanzania.
KIM KARDASHIAN Promotes Her Belle Noel Jewelry Collection
Alivyoibiwa si vitu vya kujaza mabegi, ni vichache tu lakini vyenye thamani ya kukuduwaza. Ni mikufu ya thamani, simu pamoja na pete yenye thamani ya dola milioni 4.5 aliyopewa na mumewe Kanye West.
Jumla ya mali zote ni zaidi dola milioni 10 ambazo ni kama shilingi 21,600,000,000 za Tanzania (bilioni 21.6). Fedha hizo ni mara 6 zaidi ya fedha ambayo serikali ilitenga kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo zitakazotumika kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Ubunifu.
Serikali ilitengeza shilingi bilioni 3 kwa kazi hiyo mwaka huu.
Powered by Blogger.