Mchezaji Thomas Ulimwengu aondoka TP Mazembe, afuata ndoto zake kucheza Ulaya

Baada ya kucheza misimu mitano kwenye klabu ya TP Mazembe, mchezaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu ameondoka kufuata ndoto zake kucheza Ulaya.
cbrhiyiwiaao0yh
Mchezaji huyo aliyekuwa akivaa jezi namba 28 na aliyepewa jina la utani ‘Rambo’ alichukuliwa na klabu hiyo akiwa na umri 18 kutoka AFC Academy ya Stockholm, Sweden. Akiwa na TP Mazembe, Ulimwengu amecheza mechi 130 na kufunga mabao 35.
Wakati anachezea klabu hiyo klabu nyingi zilitaka kumchukua lakini aliamua kumaliza kwanza mkataba wake na Mazembe. Aliamua kutoongeza tena mkataba na TPM. Na sasa Ulimwengu anataka kufuata nyayo za Mtanzania mwenzake Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji.
Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu alisema kupitia taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, “Kwa miaka mitano Mazembe imeniruhusu kuendelea kukua kisoka na nataka kuwashukuru wote walioniunga mkono na kusaidia kushinda vikombe wakiongozwa na Rais Katumbi na Mrs Carine, viongozi na makocha.”
Powered by Blogger.