Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea usiku wa October 19 2016 kwa
viwanja 8 kuchezwa michezo 8 ya hatua ya makundi, moja kati ya michezo
ilikuwa ukitazamwa na wengi ni katiki ya Barcelona ambao walikuwa
nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa
kichapo cha 4-0, Messi akipiga hat-trick, Arsenal nao waliiadhibu
Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil nae akipata hat
trick.

Mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia
mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye
akizawadiwa kadi nyekundu.