Ndani ya U Heard ya Clouds FM amesikika msanii Abubakari Mzuri ambaye wiki iliyopita kupitia U Heard kulikua na stori yake juu ya kudaiwa kufamaniwa na mke wa mtu. Leo mtangazaji Soudy Brown amempata Aboubakar Mzuri na kuzungumza naye kuhusu taarifa hizo.

Aboubakar Mzuri amesema kuwa hakuna ukweli wa tukio hilo na kudai kuwa suala hilo limetengenezwa na watu ili kumchafulia tu sifa yake kwa jamii huku akikataa kujibu chochote kuhusu tukio hilo la fumanizi na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la Mjomba.

Hizo ni taarifa zenu ndio zinasema hivo, kwanza namba yangu umeipata wapi? Ulitakiwa kumuuliza QS Mhonda au kunipigia kwanza mimi ujue nini kilitokea sio kukurupuka na kusema vitu ambavyo hamjui vikoje. Mimi ni mtu maarufu mlitakiwa kunitafuta kwanza huenda nilivamiwa na majambazi je?:- Aboubakari Mzuri

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top