Magic Soldier " Kingorongoro" hasema hakuna mwana Hip Hop zaidi yake, Bface bado sana


Rapper mkali wa Ile Ile, Magic Soldier almaarufu kama Kingorongoro amefunguka kwa kusema kuwa hakuna msanii wa Hip Hop ambaye amefikia levo yake na huku akidai B Face na wengine  wametengenezwa ili waje kulishika game la muziki na haoni kama wataweza kumfunika kwasasa.

Akiongea na African Mishe jumapili hii, Kingorongoro  amedai mpaka sasa hakuna msanii ambaye ameweza kumfunika katika game ya muziki na ameongeza na kusema kuwa amejipanga vizuri mwaka huu na miaka zote za uhai wake hakuna mwana Hip Hop anaweza kuyafikia levo yake huku akimtaja rapper B Face mkali wa Sisomeki ambaye anazidi kufanya vizuri kwenye game ya muziki wa hip hop kuwa hawezi kumfunika.

“ kwasasa sijamsikia yule mtu ambaye anafanya matukio kama mimi, yakuflow kama mimi kama walikuwepo ila kwasasa sioni, ivi nani amekwisha sikia watu wamezimia kwenye show, bado sijawai kusikia matukio kama hayo,” alisema Kingorongoro

Alipo Ulizwa kuhusu mwana Hip Hop anaye kubali kwasasa, msanii huyo amemtaja B Face na kusema kuwa haoni kama anaweza kumfunika,
“Lakini nawasikia, kama B face na wengine namsikia na namuona kwenye muziki huu anatengenezwa ili aishike game hii, lakini hana nguvu, sisemi hivyo kama namblock hapana, kama anataka kufaamu hilo tufanye naye nyimbo tuone nani atakae funika mwenzie, Hasomeki ila mi ni Ule ule toka enzi zile" alisema Magic Soldier Kingorongoro

Hii kali sasa sijuwi B Face ataichukuliaje hii kauli ya rapper mwenzie na je atakubali kushirikiana naye ili tuone nani mkali wa hip hop kati yawo?
Powered by Blogger.