Mtayarishaji wa muziki kutoka ‘Wasafi Record’, Lizer amefunguka kwa kusema kuwa aina ya muziki anaofanya haikupendwa na viongozi wa label hiyo.
wcb
Wasanii wa WCB wakiwa studio.
Lizer ambaye tayari ameshafanya hits kadhaa za wasanii wa WCB, amesema aliwalazimisha kuukubali muziki wake ili kuwa tofauti na maproducer hapa.
“Changamoto ambayo nilikutana nayo kwanza nilileta muziki mwingine ambao ulikuwa tofauti na wao walikuwa na muziki wao,” Lizer aliiambia FNL ya EATV. “Kwa hiyo walikuwa wanajaribu kuni-force niwe kama producer wa hapa, lakini mimi nikasema nikiwa kama producer wa hapa nitakuwa sijaleta kitu kipya natakiwa kuwa tofauti kidogo. Kwa hiyo niliwalazimisha muziki wangu na nashukuru mungu watu wameupokea vizuri na wao tunaenda sawa,”
Pia Lizer alisema siyo kweli kwamba Harmonize anamwiga Diamond kuimba ambapo amedai wasanii hao kila mmoja ana muziki wake.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top