Kwanini Tambwe ameanza kufanya collabo na wasanii wa Burundi kuliko wa nje?

Mutayarishaji pia muigizaji wa filamu nchini Burundi, Tambwe amefunguka na kile ambacho wengi wanazidi kumuuliza kuhusu filamu yake mpya ambayo anatarajia kuachia hivi karibuni akiwashirikisha ma Staa kibao wa Burundi Flava ikiwa ni pamoja na Jay Fire, Mrembo Divine, Chany Queen.

Tambwe akiwa kiongozi wa kampuni inayo usika na Uigizaji wa filamu itwayo Tambwe The Great Films, amesema kuwa ndoto yake ni kuanza kufanya kazi na ma staa wa Burundi baadae atakwenda nje ya Burundi ili kufanya kazi na wasanii wa nje.

Tambwe ametoa elimu ndogo kupitia  uzoefu wake, nini cha kufanya ili kazi yako iwe na maana na ikuletee matunda.

"cha muhimu watu wajue uje na style yako, kwa mfano unataka kufanya filamu na watanzania  halafu wewe pia una style kama ya wa tanzania, ndio maana wengi wanapenda kuiga na wanashindwa  namna ya kutoboa wanashindwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kutokana na hivyo, lazima nije tofauti na wao na pia hii ndio style yangu baadae nitaigiza na wasanii wakubwa wa nje ila nitaigiza tofauti na wao ili mashabiki wa Burundi Movie watafautishe kazi zetu".

Tuwakumbushe kuwa Kampuni Tambwe The Great Films inatarajia kuachia filamu mpya mwishoni mwa mwaka na katika filamu hiyo kuna ma staa kibao wa Burundi Flava huku pakiwa habari ya kuwa mwanamuziki wa kike Natacha na super staa Big Fizzo watakuwepo kwenye filamu hiyo ila ni habari tunazidi kuifatilia kwa ukaribu.
Powered by Blogger.