Kuna uwezekano wa kuisikia remix ya wimbo wa Salome ambayo ndani yake sauti ya Harmonize na Rich Mavoko zitasikika – hayo ni maneno ya Harmonize aliyoandika kwenye mtandao wake wa Instagram.
wcb
“Unatamani kusikia sauti yangu na @richmavoko kwenye #salome remix ……???,” ameandika Harmonize kwenye moja ya picha aliyoiweka kwenye mtandao huo ikiwaonyesha wakiwa studio. Naye Rich Mavoko hakutaka kupitwa na hilo alijazia kwa kuandika kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo kwa kuandika, “Eti unatamani kusikia ngoma yetu ya pamoja??.”
Original ya wimbo huo uliimbwa na Saida Karoli mika 16 iliyopita lakini Diamond aliamua kuurudia wimbo huo na sasa umeonekana kufanya vizuri kwenye kila kona huku ukitazamwa zaidi ya mara milini tatu ndani ya wiki moja kwenye mtandao wa Youtube.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top