Kocha wa Inter Star analaumu safu ya ushambuliaji yake baada ya kutoka suluhu dhidi ya Atletico Olympic

Meneja wa Timu ya Inter Star ya daraja ya kwanza katika Primus League Burundi, Niyonkuru Djumaine ameanza kulaumu safu ya ushambuliaji ilioonesha kiwango kibovu kwenye mchezo dhidi ya Atletico Olympic ulioisha kwa suluhu.

Timu zote mbili zilionekana kucheza vizuri zaidi ila upande wa Inter Star ilionekana vizuri katika safu ya ulinzi na kuwapa Atletico Olympic hali ngumu kupenya , lakini safu yao ya ushambuliaji ilionekana kuwa likizo kama huu mshambuliaji Abdalah.

Akiojiwa na waandishi wa habari, Niyonkuru Jumaine ameonekana kutupa lawama kwenye safu ya ushambuliaji  kutokuonesha kiwango kizuri.

"kwa kweli namshakuru Mungu kuona tumemaliza mchezo wa leo najua kama kuna mechi nyingi zinanisubiri na ninaitajika kufanya vizuri, kwa mechi ya leo naona kwa upande wa safu ya ulinzi ilikua bora sana ila kwenye ushambuliaji palikua tatizo na hii ndio itakua kazi kwangu kuandaa kwenye safu ya ushambuliaji na tunakwenda kuiweka sawa tatizo hii ili tuakikishe tumefanya vizuri mechi zinazosalia", amesma Niyonkuru Djumaine
Aidha, Niyonkuru Djumaine amesema kuwa mchezo umekuwa mgumu kwao na kwa Atletico pia huku akiongeza kuwa wameanza vyema na wamewadhibiti kwa kiasi kikubwa.

Tuwakumbushe kuwa licha ya kutoka suluhu katika mechi ya wiki ya 7, Inter Star imekuwa kileleni baada ya LLB kuambuliwa kipigo dhidi ya wabingwa watetezi Vitalo (0-1).


Powered by Blogger.