responsive ads

Kocha wa Inter star amesema baada ya kujihakikishia ushindi kwa tabu dhidi ya Magara Star

Kocha mku wa timu ya Inter Star, Niyonkuru  Djumaine amesema baada ya kujihakikishia ushindi kwa tabu wa bao moja bila dhidi ya Magara Star kwenye uwanja wa CTN mjini Bujumbura, sasa nguvu  zao wanaelekezea mechi zingine.

Amesema kutokana na hali hii ya kuwa na pointi zote 12 katika mechi 4 katika Ligi kuu Primus League huku wengi wanazidi kupatwa namshangao kwa matokeo ya timu hiyo, amesema wamejipanga na kwa uwezo wa Mungu watahakikisha wanapenya kwa kufanya vizuri mechi zinazo salia.

“Katika mpira kila kitu kinawezekana, hakuna kisichowezekana. Ligi bado ingali mwanzo tuna nafasi ya kufanya vyema, alisema kocha Mkuu wa Inter Star, Niyonkuru Djumaine

  Kocha alisema kila mchezaji na kocha anataka kuona ndoto ya kutengeneza historia inatimia, lakini kwa ajili ya kufika huko, ni lazima mawazo yao yalenge michezo zinazo salia kwa kucheza kwa juhudi. “Tunafurahi tumeifunga Magara Star ata kama mechi imeonekana kuwa  ngumu upande wetu ila tumeakikisha kupata tunacho taka na sasa tunawazia zaidi kufanya vizuri mechi zingine alisema kocha Djumaine.middle 300x250
Powered by Blogger.