Kocha Roberto Di Matteo atimuliwa kazi Aston Villa

Kocha Roberto di Matteo ametimuliwa kazi katika klabu ya Aston Villa ya Uingereza baada ya kudumu kwa siku 124 tangu akabidhiwe mikoba katika klabu hiyo inayocheza ligi ya championship.

Villa sasa wanatafuta meneja wao wa tano katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja. Walishinda mechi moja pekee kati ya 11 walizocheza ligi ya daraja la pili, ligi ya Championship, chini ya Di Matteo.
Di Matteo, 46, ambaye alikuwa mchezaji na meneja wa Chelsea wakati mmoja, aliteuliwa meneja wa Villa baada ya mfanyabiashara Mchina Dkt Tony Xia kununua klabu hiyo mwezi Juni. Villa walizomewa na mashabiki Jumamosi baada ya kulazwa 2-0 ligini Preston.
Steve Bruce na Mick McCarthy ni miongoni mwa mameneja wanaopigiwa upatu kumrithi Di Matteo. Katika mechi tano kati ya 11 walizocheza chini ya Di Matteo, walifungwa bao moja kila dakika 85.
Powered by Blogger.