Mtangazaji wa Clouds FM, Paul James aka PJ ameshtakiwa mahakamani na kituo cha redio cha EFM kwa kuvunja mkataba kinyemela.
picha-ya-pj
Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.
Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
efm-radio-page-001
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top