Kingorongoro afunguka kuwa Ashley Diva anafaa kuwa mke mwenye sifa zote


Mkali wa Ile ile kutoka Burundi, akijulikana kwa jina la Kingorongoro ambaye kwasasa anazidi kufanya vizuri na video ya nyimbo yake mpya itwayo Ile ile, ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii.

Kingorongoro yupo studio kwasasa uko pande za Master Music chini ya mikono ya producer Master Land akikamilisha ujio wa nyimbo yake mpya akishirikiana na mwanadada mrembo Ashley Diva itwayo Moyo wangu.

Akizungumzia mbele ya waandishi wa habari, Kingorongoro amefunguka kuhusu mwanadada mrembo Asheley Diva na kusema kuwa siku chache amekutana na mrembo huyu kikazi amegundua kitu kuwa Asheley Diva anafaa kuwa Mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo. Mkali wa ile ile ameongeza nakusema kuwa Ashley Diva ni mchapa kazi  na anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia kazi yake ya muziki zake kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).  

Kingorongoro amesema kuwa huwezi kuzuia hisia za muziki  unaweza kuwa msanii na unapenda kazi za msanii mwingine pia nami nimevutiwa na Ashley Diva anafaa kuwa mke anaye jituma na kuiweka familia yake kuwa imara.

Tuwakumbushe kuwa Kingorongoro bado hajafanikiwa kupata mpenzi wa maisha yake pengini hii itakuwa ni njia ya kumpata mrembo Ashley Diva licha  ya kummwagia sifa hizo zote. itaendelea ...
Powered by Blogger.