Kauli tata ya Donald Trump dhidi ya wanawake yaiponza ajira ya mwandishi

Kituo cha utangazaji cha NBC cha Marekani kimemfukuza kazi mtangazaji wake Billy Bush wa kipindi cha Today ambaye alimhoji Donald Trump miaka 10 iliyopita alipotoa matamshi ya udhalilishaji kwa wanawake.
the-new-yorker-who-is-donald-trump
Bush ambaye ni mmoja wa watu wa familia ya aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush aliingia kwenye kashfa hiyo baada ya kusikika akicheka kwenye mkanda huo wa video baada ya Trump kutoa kauli yake ya kuwadhalilisha wanawake iliyosambaa zaidi kuanzia wiki mbili zilizopita.
Kupitia taarifa iliyotolewa na kituo hicho cha NBC imesema, “Ingawa alikuwa mgeni tu [Billy] katika waandaaji wa kipindi cha Today, amekuwa na NBC kwa muda mrefu. Tunamtakia kila la heri.”
Hata hivyo mtangazaji huyo aliomba radhi siku chache baada ya mkanda huo kusambaa, alisema, “embarrassed and ashamed and that although the incident happened 11 years ago, that’s no excuse.”
Hata hivyo mke wa Trump, Melania ameendelea kumshtumu Billy kuwa ndiye alimchochea mumewe mpaka kufikia hatua ya kuzungumza mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Mpaka sasa baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wameonekana kutomuunga mkono Trump kutokana na kauli zake.
Powered by Blogger.