Judie Caelle Licha ya kuwa Mtangazaji wa radio La Colombe pia ni muigizaji wa Burundi Movie

Mtangazaji wa radio la Colombe inchini Burundi, Gahimbare Judie Caelle, ameamua kurudi kwenye tasnia ya uigizaji wa filamu baada ya miaka kadhaa kusimamisha na kujifunza vizuri utangazaji.

Dada huyu asiyeishiwa matukio, aliyepata umaarufu tangu miaka za nyuma, pale alipokuwa muigizaji wa filamu na amezidi kupata umaarufu kwenye Utangazaji katika Kipindi cha Buja Actor kinacho ongelea kuhusu filamu na Ahabona Moment kinacho ongelea muziki, muonekano wake umebadilika kwa kiwango kikubwa sana.
 Judie Caelle ameanza kazi ya Uigizaji tangu mwaka wa 2005 baada ya miaka mitatu amesimamisha kwa  kujifunza vizuri utangazaji na katika kipindi chote amekuwa kama mushahuri mkubwa wa waigizaji na kufanikiwa kusaidia kuigiza katika filamu moja itwayo House in Hell.

Mtangazaji huyu ameamua kurudi kwenye game ya uigizaji kwa mara nyingine tena huku anatarajia kuachia filamu yake mpya itwayo 7th Days ambayo atashirikiana na ma staa kibao.
Akiongea na africanmishe, mwanadada huyu ambaye ni mtangazaji wa radio la Colombe, amesema kuwa
"wengi watafikiri pengine naacha utangazaji, najua wananipenda kama mtangazaji na nitasalia kama mtangazaji na pia watanipenda kama muigizaji pia ila sijaacha kitu nitaendelea kuwa mtangazaji kwenye vipindi vyangu. Uigizaji is my first time kwa hiyo mashabiki zangu na mashabiki wa Burundi Movie mtakuja kuona kazi yangu nyingine nzuri ninaimani mutaipenda"
Powered by Blogger.