Jinsi ya Kuficha Picha na Video za WhatsApp Zisionekane Kwenye Gallery

Kuna wakati inatokea umetumiwa picha kwenye programu ya WhatsApp na picha hizi mara nyingi inatokea zinajidownload zenyewe hivyo husababisha picha hizo kuonekana moja kwa moja kwenye Gallery ya simu yako, hii imekua ni tatizo na mara nyingi imekua ikileta kutofautiana sana baina ya watu mbalimbali sasa kama wewe umekua ukipata matatizo kama haya leo ni mwisho kwani leo tunaenda kujifunza namna ya kuficha picha na video za whatsapp zisionekane kwenye Gallery ya simu yako. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuwa na ulinzi wa picha zako na vile vile utakua na uwezo wa ukiziona picha zako hizo kwenye programu ya WhatsApp pekee na sio sehemu nyingine yoyote kwenye simu yako.
Kwa kuanza basi ili kuhakikisha picha zako hazionekani kwenye Gallery ya simu yako unatakiwa kuwa na simu yako ya Android au simu nyingine yoyote ile yenye uwezo wa kuwa na programu ya kuangalia mafaili yani (File Manager) na vilevile hakikisha programu ya WhatsApp ipo vizuri kwenye simu yako hiyo unayotaka kufanya zoezi hilo. Basi kama utakua umefuata hayo yote basi utakua uko nusu ya kuwezesha picha zako za whatsapp zisionekane kwenye Gallery ya simu yako.
Basi hatua ya kwanza chukua simu yako na fungua programu ya (File Manager) kama simu yako haina programu hiyo ingia (Play Store kama unatumia Android) na kisha tafuta programu hiyo kwa kuandika maneno “File Manager” tafuta programu inayo kufaa kisha (install) kwenye simu yako
Powered by Blogger.