Jeff Kashindi mchezaji wa Inter Star awataka mashabiki wa timu yake kutulia dhidi ya LLB

Mchezaji wa timu ya Inter Star, Jeff Kashindi amewataka mashabiki wa timu yake kutulia siku ya mechi dhidi ya timu yake ambayo ameichezea msimu uliyo pita LLB.

Jeff ni mchezaji mwenye kipaji cha haina ya pekee kwasababu anauwezo wakucheza sehemu nyingi uwanjani kadiri ya kocha anavyo mpanga. Baada ya kuisadia klabu yake mpya Inter Star kuwa kileleni na pointi zote 12 katika mechi 4 ambayo amejiunga msimu huu akitokea katika timu LLB na awali amewahi kuichezea inter Star, amewambia mashabiki wa timu hiyo kutulia dhidi ya LLB hapo jumamossi tarehe 08 mwezi huu saa kumi kamili.
Jeff Kashindi ameiambia Mishe Mishe kuwa LLB naipenda ila kwasasa naitumikia Inter Star na siku hiyo anawaomba mashabiki wa timu yake kutulia na kutokuhofu mechi ya jumamossi dhidi ya LLB, kwani ni mechi ya kawaida kama mechi ambazo amezifunga.

Homa ya mechi hii kati ya timu zote ambazo kwasasa zinaongazo Ligi imepanda mpaka kwa mashabiki wa timu zote mbili lakini Jeff kashindi alisema haoni kitu chakumuhumiza kichwa na kuwa ni mechi ya kawaida huku akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi washuhudie mechi hiyo.

Powered by Blogger.