Ivory Coast : Gervinho sasa basi kwa Can 2017


Mshambuliaji wa Hebei China Fortune, yupo katika hali ngumu baada ya tarifa kuthibitisha kuwa itakuwa vigumu sana kumuona Gervinho kwenye Kombe La Mataifa ya Afrika.

Kwa mjibu wa France Football, Gervinho ana majeruhi  katika goti lake la kushoto  na amejielekeza Ufaransa kupata vipimo vya ziada hii itampelekea kukaa nje ya viwanja miezi sita.

Mchezaji wa zamani wa As Roma atakosa Kombe la Mataifa ya Afrika itayofanyika kuanzia Januari 14 hadi Februari 5, 2017.

Hii ni pigo kubwa ya Michel Dussuyer na Ivory Coast  kwa kumpoteza moja wa washambuliaji aliyechangia ushindi katika fainali la kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Powered by Blogger.