Huyu ni Msanii Mwingine Kutoka Afrika Aliyesaini na Lebo ya Sony Music

Ijumaa ya tarehe 21 October 2016, Afrika kusini ikiwa ni tawi la Sony Music Entertainment, kampuni ya masuala ya Entertainment kwa upande wa Afrika, ilitangaza kumsaini msanii mwingine ndani ya lebo hiyo, Ycee ambaye anafanya kazi na lebo ya Tinny Entertainment.

Mkataba aliosaini YCEE unaonesha kuwa Sony Music watasimamia albam yake ya kwanza na ngoma zake zote zitakazoanza kutoka pamoja na usambazaji wake kuanzia sasa zitakua chini ya mwavuli wa Sony Music. Kwa shavu hilo inamaana kuwa Ycee anaungana na Nigerian superstar Davido, pamoja na Alikiba kwenye familia ya mastar kutoka Afrika walikula deal la Sony Music.

Kwa mujibu wa Michael Ugwu, General Manager wa Sony Music West Africa amesema “Nina furaha kubwa sana kuwakaribisha Tinny Entertainment pamoja na msanii wao Ycee ndani ya familia ya Sony Music Entertainment West Africa. Nimekuwa nikishuhudia team hii ikikua kwa haraka kwenye miaka ya karibuni na nimeshangazwa na jinsi walivyoweza kufikka hapa, Ycee ni msanii mkali sana wa Hip Hop barani Afrika na muda sio mrefu atakua kwenye level za mbali sana.”

Kwa upande wa Arokodare ‘Tinny’ Timilehin, ambaye ni CEO wa Tinny Entertainment, amesema

“Tuko na furaha sana kwa upande wetu na msanii wetu Ycee. Huu ni uthibitisho kuwa tumefanya kazi kubwa sana mpaka kufikia hapa. Na katika kuonesha furaha yake juu ya deal hiyo,
Powered by Blogger.