Huu ndie Muimba Taarabu anazidi kuitangaza Tasnia ya taarabu ya Burundi Duniani Pote

Taarabu ni muziki wenye asili ya pwani, na kuna taarifa zisizo rasmi ambazo zinasema kuwa muziki huu ulianzishwa miaka themanini "80" iliyopita, muziki huu umekuwa ukipitia vipindi tofauti mpaka sasa kufikia kuitwa "Modern Taarabu", kuna watu wengi maarufu walioweza kuitangaza taarabu mpaka sasa tunaitambua na nchini Burundi ni Papa Fololo.

Papa Fololo ni raia kutoka Burundi, mtoto wamjini wilaya ya Buyenzi18\20, na amezaliwa katika hospitali ijulikanao kama Hopital Rrince Regent Charles. 
Ameanza kazi ya muziki 1987 katika band ya Chany 10\19, ni mtoto aliye lelewa na mama yake mzazi ambaye kwasasa ni marehemu pia alijiunga na Band mbalimbali ikiwemo Super Star, Super Democratie, Jasmini pia kazi zake zilifanya vizuri mpaka zikasikika hadi Tanzania.

1994, nchini Tanzania amejiunga na Band ya Magereza, Maqoiz du Zaire ya Tanzania na wakaianzisha Band ya 5 Star akiwemo Papa Fololo mwenyewe, Abdoul Misambano, Hussein Kibao, Ally Tajiruna na wengineo.
1997, Papa Fololo amejiunga na Afrigo Band ya mjini Nakasero Kampala.
2011, Papa Fololo ameteuliwa kama kiongozi wa band ya Makungu Jazz ya mkoani  Kigoma, Band ilikua inausika na mchanganyiko wa muziki hapo akiwa kama mpiga kinanda mahiri  wa Band hiyo.

2015,03 Papa Fololo ametuwa nchini Canada kama mwana nchi mpya wa nchi hiyo, 05, 2015 ameanzisha Band  ya Muziki wa Taarabu ya kizazi kipya kutoka Burundi na tayari Band hiyo imekwisha rikodi  video 3 ( Moyo Ukipenda, Mama nihurumiye na Msaliti) na Audio 16.
Tuwakumbushe kuwa Papa Fololo ni muimbaji wa taarabu ambae kwasasa anazidi kupeperusha bendera ya Burundi nchini Canada kwa tamasha mbali mbali huku akijulikana sana nchini hapo kupitia kazi yake itwayo Mama nihurumie

Powered by Blogger.