Hakimu wa mahakama ya wilaya Arusha akataa ubabaishaji wa kesi

Na.Vero Ignatus Arusha.

HAKIMU wa Mahakama ya Wilaya Arusha,Patricia Kisinda amekataa ubabaishaji katika kesi ya aliyekuwa           Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA) na mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bernard Murunya (65), na kuamuru upande wa utetezi kumaliza utetezi wao ndani ya siku mbili zilizopangwa na mahakama.

Akizungumza mahakamani hapo, Hakimu Kisinda amesema kesi hiyo imekaa mwaka mzima, sasa anataka iishe na sio kuiahirisha kila siku.

“Nataka tarehe itakayopangwa na mahakama oktoba !( na  utetezi mumalize sitaki tena mambo mengine,”alisema

Kabla ya kuzungumza hakimu huyo Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Hamidu Simbano akisaidiana na Rehema Mteta, aliiambia Mahakama hiyo wapo tayari kuendelea na utetezi.

Baada ya kuzungumza hivyo Wakili upande wa Utetezi,Jafari Liindi aliomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa sababu Wakili anayeongoza upande wa huo, Boniface Joseph kulazwa hospitali ya Aicc.

 Nimekuwa zamu ya utetezi wa mshatakiwa aliyekuwa  Meneja wa
Utalii wa Mamlaka hiyo, Veronica Funguo, baada ya Murunya kumaliza utetezi wake juzi.
Baada ya kumaliza ufunguo mshtakiwa mwingine atakayetoa ushahidi wake ni aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha na utawala wa Mamlaka hiyo, Shad Kiambile.
Hakimu Patricia Kisinda wa Mahakama ya wilaya ya Arusha,anayesikiliza
kesi hiyo tayari amepokea ushahidi wa upande wa  Jamhuri ambao
walileta  mashahidi nane na vielelezo kadhaa.

Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri  unawakilishwa na Mawakili wa
Takukuru mkoani  Arusha, Wakili  Rehema Mteta na Hamidu Sembano,wakati
 Murunya  na wenzake wakitetewa na John Materu na Boniface Joseph.

Watuhumiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao ha
kuisababishia mamlaka hiyo upotevu wa Dola 66,890 ikiwa ni pamoja na
kuipatia kampuni ya Cosmos fedha hizo kabla ya kutoa huduma, kinyume
cha Sheria ya matumizi ya fedha za umma.
Powered by Blogger.